Monday, June 20, 2011

KITU CHA BUSU LA TUPA T.I.D NDANI...

Kitu cha BUSU..ETI ... DAH !!!!!....
Staa wa Bongo Fleva, Khaleed Salum Mohamed ‘TID’,  (pichani)amekamatwa na kuswekwa rumande, mashtaka nyuma yake yakiwa ni kumbusu bila hiari, mrembo Fatma Sahil, mkazi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam.

TID, anadaiwa kwamba, Juni 16, mwaka huu, saa 7:00 usiku, katika eneo la American Chips, Kinondoni, alimvamia Fatma, akamvutia kwenye gari kisha kumbusu shavuni pasipo makubaliano yoyote.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa TID alikamatwa juzi (Jumamosi) na kuswekwa selo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar na katika kitabu cha kumbukumbu za polisi (Report Book ‘RB’) namba ya kesi ni OB/RB/292/2011, SHAMBULIO LA AIBU.

Paparazi wetu alipofika kituoni hapo juzi, hakuweza kumfikia TID, kwani alielezwa yupo mahabusu kwa wakati huo.

Mpaka saa 7:00 mchana juzi (Jumamosi), TID anayemiliki Top Band alikuwa bado ameshikiliwa kituoni hapo, akisubiri kutoa maelezo ili kama ni dhamana ijadiliwe kuanzia hapo.

Aidha, paparazi wetu akiwa kituoni hapo, alimuona Fatma lakini haikuwa rahisi kuzungumza naye kwa sababu aliingia kwenye mazungumzo na askari anayepeleleza shauri lake.

Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni juzi, TID alikuwa bado yupo mahabusu.

No comments:

Post a Comment