Thursday, June 30, 2011

WATANZANIA WANAOTESA KWENYE TUSKER PROJECT FAME ALL STAR

                                           Hemedi  akiwa on stage siku ya ufunguzi.

Monday, June 27, 2011

AFRIKA YAPATA FURAHA BAADA YA KOKO MASTER D'BANJ NA 2FACE KUPATA TUZO ZA B.E.T


Kati ka ile category ya (BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA)ambao walikuwa wanawania wasani kama SITA hivi toka barani afrika ,akiwemo D-Black (Ghana) , Fally Ipupa (DR Congo),Angelique Kidjo (Benin),Teargas (South Africa) Ebana mzigo ume dondoka kwa wana toka pande za NIGERIA "OGA BOYS"..DBANJ na 2FACE ndio wameibuka washindi wa hii tunzo ya B.E.T...

Thursday, June 23, 2011

DMX AMEFAYA (DISS) SWAGGA YA DRAKE...

Licha kuwa jama bado yupo ndani (kitu cha jela)...X anasema  mingoni mwa watu ambao hategemei kupiga nao kazi ni DRAKE. DMX ansema uwa style ya hawa washkaji wa YMCMB uwa haielewi hata kidogo...na sio kwa roho mbaya ila anajaribu kkuimeza ameshidwa....

Wednesday, June 22, 2011

IMEKUWA CONFIRMED JUMA PILI HII SHAAA NDANI YA BBA AMPLIFIED STAGE

Shaaaa confirmed kukisanuwa juma pili hiiii ndani ya BIG BROTHER AMPLIFIED...

WAKURUGENZI WA STUDIO HOUSES BONGO RECORDS NA B-HITS WAKUTANA...KUNANI..!!!!

HAWA WASHKAJI VP..KUSHOTO NI HERMY B, KULIA P'FUNK MAJANI !!! KUNA MZIGO WANAUNYONGA KWA PAMOJA AU...TEGEA SKIO UTAJUA WASSUUUUPP...!!!!

ELEPHANT MAN NDANI YA TANZANIA a.k.a BONGO LAND

Mkali wa dancehall  ELEPHANT MAN tokea pande za JAMAICA yupo nchini kwa kutupia show moja matata...so kaeni tu attention wapenda ngoma za ki JAMAICA....

MWANA DADA SHAAAA KUTIMBA KWENYE BIG BROTHER AMPLIFIED STAGE..

MDADa shosti kutokea kwenye kitu cha label ya mjay recods SARAH KAISI ...almaarufu kama "SHAA"
alie kudondoshea mizigo kama, ZAMU YANGU, MTIMA NYONGO,SHOGA na saivi ana mzigo wake unao kimbiza kitaaani CRAZY,ame kula kitu cha shavu kwenda ku perform kwenye sunday show ya big brother africa amplified...ni bongela shavu..ila SHAA hajafunguka kuwa ata perform juma pili ipi...!!! so to stay tuned in na babkubwa 1 xtar kuweza kujua kama itakuwa aje...

SIKU YA LEO J'5 professor jay yupo kwenye set ya kideo chake -KAMA IPO

professor jay yupo busy kutengeneza kideo cha mzigo wake mpyaaa... unao kwenda kwa jina "KAMA IPO IPO" Babkubwa 1 xtra imecheck naye na akasema kuwa mashabiki wake kupitia kurasa zake zote mbilli  face book pamoja na Twitter ,waliomba kideo ...so anacho fanya ni kuwasikiliza na kuwatengenezea hiko kideo...mtu mzima toka visual lab.."ADAM JUMA" ndio anasimamia mpango mzima...

JAFFARY NINI TENA JOMBAAAA....

Msanii  Jahffarai naye amesomeka kwenye ukurasa wake wa facebook akimjibu Mr II kwa style hii...
 
"Nikiwa km m1 kati ya wasanii wengi sana tuliosoma mbeya, naamini kuwa  jiji la Mbeya ni kitovu cha hip hop nchini,
sasa mr 2 uctake kuleta chuki zako binafsi ukataka kuwashika masikio watu wa mby ili kuzuia FIESTA, nawajua wakazi wa Mbeya ni wajanja na hawawezi kukubaliana na upuuzi wako hata cku 1.. Lete hoja za msingi bungeni km wenzako wakina Zitto cyo unaleta mambo ya uchochezi na chuki!!!"

Monday, June 20, 2011

Washkaji wakutana kwenye set ya MEN IN BLACK 3

Jayz alidondoka kwenye set (eneo la ku shoot movie) ya Will Smith mpya iitwayo "MEN IN BLACK 3" jigga aliamua tu kumtembelea mwanae acheck jinsi gani mchizi anaigiza.  watu wengi sana hawajuhi kama WILL SMITH ALIKUWA KWENYE MZIKI WA RAP kabla hajadondoka kwenye industry ya muziki..check kitu cha picha hapo chini..

sean kingston apata nafu...

kwa maara ya kwanza watu ambao wanam follow sean kingstone kwenye mtandao wa twitter wamefanikiwa kumuona alivyo ki hali yani tangia ile siku ya ajali ya ki boat pande za miami...kingstone amesema yuko poa kwa sasa na hali ina kwendelea vidhuri lakini pia kingstone amesha ruhsiwa toka hospitali so yupo maskani kwake kwa naeno yake mwenyewe KiNGSTONE ANASEMA HIVI...""Feeling alot better!  "GOD IS GREAT! Thanks for all the prayers and support! Love you ALL!”"....chungulia kitu cha picha hapo kati....

Hakuna cha tamasha la fiesta kwa mbeya mheshimiwa Joseph "sugu' Mbilinyi asema


Mbunge wa Mbeya Mjini Kupitia Chama cha Chadema Leo kupitia Page yake ya Facebook Ameandika ujumbe ambayo unapinga ufanyikaji wa Tamasha kubwa la Fiesta. Joseph Mbilinyi ambaye pia ni mwasisi wa mziki wa Bongo Flava aliandika Ujumbe Unaosomeka Hivi "

KITU CHA BUSU LA TUPA T.I.D NDANI...

Kitu cha BUSU..ETI ... DAH !!!!!....
Staa wa Bongo Fleva, Khaleed Salum Mohamed ‘TID’,  (pichani)amekamatwa na kuswekwa rumande, mashtaka nyuma yake yakiwa ni kumbusu bila hiari, mrembo Fatma Sahil, mkazi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam.

TID, anadaiwa kwamba, Juni 16, mwaka huu, saa 7:00 usiku, katika eneo la American Chips, Kinondoni, alimvamia Fatma, akamvutia kwenye gari kisha kumbusu shavuni pasipo makubaliano yoyote.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa TID alikamatwa juzi (Jumamosi) na kuswekwa selo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar na katika kitabu cha kumbukumbu za polisi (Report Book ‘RB’) namba ya kesi ni OB/RB/292/2011, SHAMBULIO LA AIBU.

Paparazi wetu alipofika kituoni hapo juzi, hakuweza kumfikia TID, kwani alielezwa yupo mahabusu kwa wakati huo.

Mpaka saa 7:00 mchana juzi (Jumamosi), TID anayemiliki Top Band alikuwa bado ameshikiliwa kituoni hapo, akisubiri kutoa maelezo ili kama ni dhamana ijadiliwe kuanzia hapo.

Aidha, paparazi wetu akiwa kituoni hapo, alimuona Fatma lakini haikuwa rahisi kuzungumza naye kwa sababu aliingia kwenye mazungumzo na askari anayepeleleza shauri lake.

Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni juzi, TID alikuwa bado yupo mahabusu.

Friday, June 17, 2011

JUSTIN TIMBERLAKE AMCHOMOLEA JIGGA KUPIGA NAYE KAZI..

Kama utakuwa una kumbu kumbu nzuri utajua Justin sio msani wa kwanza kumchomolea JIGGA kupiga naye kazi, ila mwana dada SADE toka pande za wingereza pia naye amesha wahi sema kuwa hana mzuka wa kupiga kazi na chali huyo toka Brooklyn nchini Marekani...Na SASA bwana mdogo ambae pia sio kivile kimziki saivi ...jama amejikita zaidi kwenye upande ule wa "HOLLYWOOD" kwenye industry ya kitu cha movie...na kama ulibahatika kuicheck movie moko "SOCIAL NETWORK" amabayo ilikuwa inazungumzia mpafango mzima wa kitu cha FACEBOOK... utakuwa umemcheck Justin Timberlake... "J.T" .Justin Timberlake amesema hana mazuka  kabisa kupiga inshu na JAYZ..Hayo ameyasema "JT" alivyo kuwa anahojiwa na "VANITY FAIR" Magazine...jama amefunguka KUWA kipindi cha nyuma alimuomba Jigga wapige kazi pamoja akazinguwa, akamwambia eti mda hauja kaa sawa labda kitu cha next time..ila "JT" alimindi...akamjibu JAYZ "JIGGA" kuwa sifanyi kazi kama unavyo taka wewe...so mda umefika na Jayz anataka kupiga kazi na mchizi ila mchizi amemchomolea ....sasa hapa kulikoni..."JT" analipiza kisasa au ...!!!!!!!!

SENTI 50 ASEMA KAMA YEYE NA LABEL YAKE HAWAFIKIII SOLUTION..ANAWEZA ASIACHIE ALBUM YAKE MWAKA HUU

Juzi kati mwana alikuwa na kikao na label yake ambayo ni "INTERSCOPE" lakini kulitokea kuto elewana na label juu ya lini mzigo wake unatakiwa kuuachiwa.sasa jana mchiz ikatupia kwenye twitter page yake maneno haya..."hawa washkaji siwaelewi kabisa kama vile wanatembea ki slo motion na kazi zangu...lakini tuspofikia solution mzigo naweza nisiuachie mwaka huu" Hayo ndio manen toka kwenye twitter page ya mshkaji..na pia mwana anamalizia kwa kusema huu ndio mzigo wa mwisho ntakao fanya na interscope so.. wafanye mpango waamke kutoka usingizini...

Thursday, June 16, 2011

Mzigo wa Gangster kutoka kwa Chegge na Temba kutegemewa kuwa wa kimataifa zaidi

Wasanii wawili kutoka katika  Kundi la Tmk Wanaume Family chini mkubwa Fella, Mh Temba na Chege Chigunda, wakimshirikisha Feroozi wanatarajia kumaliza video ya wimbo wao wa Kama ni Gengster, hivi karibuni chini ya Adam Juma wa Visual rab Rec.
Akiongea na Babkubwa1xtra, mkubwa Fella, anasema video hii wanataka iwe ya kimataifa zaidi.

Wednesday, June 15, 2011

STEVE NA MZEEE WA MA FREESTYLE NGWEA NO MORE KITU CHA LABEL KWA ZIZZOU

Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za wasanii hao kama kurekodi nyimbo, kutengeneza albamu, kusimamia mauzo, utengenezaji wa video na mavazi. Wakati wasanii hao wanamaliza mkataba na Zizzou Entertainment, wimbo wa Don’t Give UP waliorekodi kwa pamoja, unabamba ile mbaya katika vituo mbalimbali vya televiseni na radio nchini. Pia Ngwea, Blu na Diamond wanatarajiwa kuonekana runingani na kusikika redioni soon kwenye kazi yao ya mwisho waliyoifanya nakampuni hiyo.

2pac Angekuwa anatimiza miaka 40 LEO

mashabiki wa Beyonce wanguuka ovyo wakati walivyo kutana naye pande za wanja wa ndege

mafans wa Beyonce wamemshangaza ,baada kukutana naye pande za "NICE" airport wanja wa ndege nchini ufaransa...na kila mtu (mshabiki)kutaka kupiga naye kitu cha picha...DAH !! mmoja wao kama unavyo check kwenye picha hakwamini kabisa kama anamcheck Beyonce na macho yake...alikula kitu cha mwanguko mkubwa hadi chini...mzazi ushamba huwo tulikuwa tuna hisi kama upo Africa ....kumbe hadi mtoniiii...?????? Beyonce Alikuwa pande hizo kwa ajili ya shows kadha... na pia ali sindikizwa na mama yake mzazi mrs Tina Knowles...

Tuesday, June 14, 2011

MWANA DADA JULIANA KURUDI KAMA JUDGE WA TUSKER ALLSTARS

Mwana dada Julianna amekula shavu kwa maara nyingine tena kuwa mmoja wa ma Judge wa mashindano yale ya ma vocal za kimzimiziki (TUSKER PROJECT FAME) lakini kama tulivyo kwambia juzo kati ni kwamba kwa mwaka huu mashindano hayo yataitwa "TUSKER ALLSTARS"..llakini pia licha ya hivyo mdada huyo pia yupo nominated kwenye tunzo za nchini Nigeria ziitwazo "N.E.A" za mwaka 2011.(NIGERIAN ENTERTAINMENT AWARDS) Na kwa mwaka huu zitafanyika tarehe 4 mwezi wa Septemba pande za  Sharp Theatre in New York, nchini marekani...Juliana yupo nominated kati ka category ya Pan African Artist/Group of the Year. watu ambao anawania nao tunzo hii ni pamoja na msani kutoka pande za DRC CONGO Fally Ipupa, R2Bees, Winky D Awilo Longoba, na  VIP

WIZ KHALIFA AMINDI KUTO PEWA HESHIMA LICHA KUWA NI STAR MKUBWA

Juzi kati wakati mwana WIZ KHALIFA kadondoka pande za Duka la pamba huko mita ya Beverly hills liitwalo "BARNEY'S" na kipenzi chake alie mdaka toka kwa rapper Kanye west shostito.."AMBER ROSE" , hajapewa heshima iliyo stailli .wenye Duka walihisi mwana ni mmoja wa wahuni wa hapo kitaani, so walikuwa wanamchungulia mara kwa mara asije akaiba vitu,...DAH !!! kitu ambacho kilimsababisha kujihisi vibaya kuwa kweli kuna watu ambao hawamfahamu ulimwengu huu...hata kama mchizi alikuwa ametumia kiasi kikubwa tu ..cha mabovu kumnunulia AMBER ROSE demu wake kiatu ckenye thamani ya dolla kumi na sita elfu..($16,000)

MWALIMU Asimamishwa KAZI KWA KOSA LA KUONYESHA KIDEO CHA WIMBO WA EMINEN

Mwalimu mmoja anayejulikana kwa jina la Sarah Jordan..pande za marekani jimbo la Massachusetts amejikuta anasimamishwa  kazi kwa mda mara baada ya kukutwa ana onyesha wanafunzi wake wa shule ya msingi darasa la saba (Grade 7) kideo cha ngoma ya Eminem inayo julikana kama "SUPERMAN"..polisi pia imeingilia kati na kusema wanatafuta details kuona kuwa ni version gani alie waonyesha wanafunzi hao..ikijulikana kuwa ni ile ya "EXPLICIT" Kwa maana ya kwamba yenye mambo ya kikubwa ,basi na polisi watamfungulia mashtaka walimu huyo mwenye jina la Sarah Jordan..

MSHINDI WA TUSKER ALLSTARS KUPANDA JUKWANI NA WAMAREKANI USHER NA KERI HILSON

Taarifa zilizotufikia ni kwamba atakae bahatika kuwa mshindi wa season mpya ya Tusker project ambao imepewa jina la "TUSKER ALLSTARS",Ata perform  na wanyamwezi "Keri Hilson" Pamoja na "Usher Raymond" siku ya tarehe 20 Agosti 2011.pande za "CARNIVAL GROUNDS"jijini Nairobi...

miongoni mwa washiriki walio tajwa kupata shavu hilo ni, mshindi wa season three ambae ni mchizi toka pande za Rwanda ALPHA,Mwengine ni MKenya Bernard Nganga anaejulikana kama ‘Ngangalito’  Patricia Kihoro, Mshindi wa Season ya pili Tanzanian heartthrob Hemedi Suleiman, Peter Msechu pamoja na mshindi wa season four , Davis Ntare ..Hawa ndio wana walio bahatika kuwa kwenye hiyo orodha ya "TUSKER ALLSTARS"

Monday, June 13, 2011

ETI TEMBA HAIIMBII MZIKI WA KIHUNII...!!!!

Toka pande  za TMK, Amani Temba 'Mheshimiwa Temba' anatanabaisha kuwa muziki wake si wa kihuni na kwamba unafundisha maadili bora kunako jamii. 
 
Temba, ambaye pia ni kiongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family..alikaririwa kwenye moja ya kona alizobanwa na kusema "Kiukweli mazee si kwamba najitetea, ukweli ni kuwa muziki wangu si wa kihuni kama watu wanavyosema, unaongoza kwa kurekebisha jamii huwezi kuamini."

Taarifa kutoka darhotwire .....

BEYONCE ALA SHAVU LA GAZETTI LIITWALO "W"

Mwana dafada huyo ambae tuna wait mzigo WA album yake mpya wa "4"...ambao pia badhi ya ngoma zilizopo kwenye album  zili vuja a.k.a leak...Beyonce Kupitia mafanikio yake kimuziki na kukbalika na ma fans kibao, ametupiwa shavu la kuwa cover girl wa "W"magazine Toleo la mwezi wa saba JULY..

WANA TOKA PANDE ZA YMCMB KUTIMBA NA KUTUPIA PERFORMANCE KWENYE TUNZO ZA B.E.T 2011

Wakali wa hip hop na Rap toka young money cash money DRAKE pamoja na LIL WAYNE wata timba na kusanuwa KITU CHA LIVE PERFORMANCE kwenye zile tunzo kali za hip hop ulimwengu mzima zinazo andaliwa na kituo cha television. BLACK ENTERTAINMENT TELEVISION. Almaarufu kama "B.E.T"..tunzo hizo zita go down siku ya TAREHE 26 MWEZI Hwa sita..Taarifa Hiyo imetolewa na Executive vice president wa kituo hicho cha B.E.T bwana Steven Hill kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter kama Breaking NEWS..Lakini pia licha kuwa washkaji wata tupia performance, wapo pia kwenye mapendekezo ya category ya wasani bora wa kiume kwa upande wa HIP HOP..."BEST MALE HIP HOP" kwa maana ya wote wawili WEEZY na DRAKE...

Issue itakuwa pande za  Shrine Auditorium kule  Los Angeles, California...june 26 2011

MKE WA JA-RULE AKANUSHA TAARIFA ZINAZOZAGA MTAANI ...

Mke wake Ja-rule anaejulikana kwa jina la Aisha Atkins, amekanusha habari zinazo dai kuwa wakati mchiz anaanza kutumikia kifungo chake cha miaka mi miwilli juni 8 mwezi huu wa sita, hakuaacha mabovu yeyote kusaidia familia..

kwa maneno yake mwenye anasema "jama alijipanga vyema wakati hajatimba ndani na kuhakikisha kuwa hatupati shida kwa kitu chochote kinacho husu hella."...so kwa kumalizia Aisha ameomba watu wasiwe wanasambaza habari sizo na ukweli wowote..Ja - rule ni baba familia ambae atafanya chochote kuona kwamba sisi wana familia yake tuko salama..

mwisho kabisa anasema Aisha Atkins kuwa, Tunamuombea kwa mungu Ja - rule amalize mda wake bila makosa yeyote akiwa jella  ..



WEMA AANGUKA...!!!

Huku akiandamwa na kesi juu ya kesi, Miss Tanzania 2006/07 anayewika kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Wema Abraham Sepetu (23), ameanguka ghafla na kuzimia kisha kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilijiri jijini Dar es Slaam Ijumaa iliyopita ambapo mnyange huyo alitakiwa kutimba katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, kwa ajili ya kesi inayomkabili ya kutoa lugha chafu na kumtishia maisha mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian.

Ilidaiwa kwamba, akiwa njiani kuelekea kituoni hapo, Wema alianguka na kuzimia baada ya kupewa taarifa kuwa askari wa Kituo cha Magomeni, Dar walikuwa wamemuwekea mtego mahali hapo ili kumnasa kwa soo lingine jipya.

Ijumaa Wikienda ambalo lilikuwa limeweka kambi kituoni hapo, lilifanya kazi yake na kugundua kuwa, kulikuwa na mapaparazi kutoka chombo kimoja cha habari (Siyo Global) waliokuwa wakimsubiri Wema atimbe mahali hapo ili kupata picha za tukio lingine la kukamatwa.

Katika kuwadodosa mapaparazi hao, ilidaiwa kuwa, kuna jamaa mmoja jina halikupatikana aliyefungua kesi mpya akidai kutapeliwa simu na mrembo huyo.

TUKIO LA KUZIMIA
Akifunguka juu ya tukio la kuzimia, Wema aliyefunika ajabu kwenye Filamu ya The Diary alisema kuwa alipokea ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani kwamba, kuna kila dalili akakamatwa kwa ishu nyingine.

“Kusema kweli baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi nilipozinduka nikajikuta hospitalini,“alisema Wema.

UJUMBE WA KUJIUA WASAMBAA
Mara baada ya kurejea katika hali yake ya kawaida, Wema aliandika ujumbe wa kukata tamaa ya maisha katika ukurasa wake kwenye Mtandao wa Facebook ulioibua hofu kwamba huenda akajiua kutokana na matatizo yanamwandama.

Katika hilo, Ijumaa Wikienda lilimuuliza undani wa ujumbe huo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Niliandika ujumbe wa kuyachoka maisha kwa sababu nilikuwa na hasira sana, nilihisi nasakamwa bila sababu yoyote.

“Nashukuru watu wengi waliniandikia meseji wakiniuliza kwa nataka kujiua, niliwaambia nilifikiria hivyo kwa sababu kila siku naona kama kuna kitu nimemkosea Mungu ‘so’ ni bora nipumzike.

“Nisaidieni kuwaambia mashabiki wangu wasinichukie, nawaahidi zawadi ya filamu yangu mpya ya The Diary itakayoingia mtaani mwezi huu.”

Kama Wema angetiwa tena mbaroni kwa soo la simu, ingekuwa ni mara ya nne kutimba polisi ndani ya kipindi kifupi cha ya miezi miwili. 

taarifa toka global publishers...

Sunday, June 12, 2011

KAMANDA WA BONGO RECORDS ANA SOMESING TO SAY ...LOL...

Kwa miaka ya nyuma alijulikana kama Kinywele kimoja mkali wa midundo wakati mpafango mzima wa bongo fleva unaanza,prodyuza P-Funk ndio anataka kurudiii kwa style ileee! nasema hivyo kwasababu tayari mtu mzima kafanya bonge moja la track liitwalo 'JIMWAGE'.
Unajua kwanini? kwasababu mara ya mwisho P-funk kufanya kazi na wasanii Juma Nature, Kr na Dollo ni kipindi kirefu sana kimeshapita....kama unakumbuka ilikuwa ni enzi zileee when music was music hahaha.
Kwahiyo kwa taarifa yenu Bongo records chini ya P-funk Majani ndio washatoka na niliowataja hapo juu..unakumbuka walikua wanaitwajeee....ni'WACHUJA NAFAKA'.

Sasa sijui Majani ndio karudi au Wachuja ndio wamerudiii! Kazi kwenu 

FABOLOUS ATAJA MZIGO WA ALBUM UNADONDOKA LINI..

Mzee wa Ngoma ya "you will be killin 'em" Fabolous ,kutoka pande za brooklyn New york...ametajja kuwa album itadondoka mwezi wa tisa(september 13) mwaka huu 2011..mzigo utaitwa hivi ....

"Loso's Way 2: The Rise To Power"..mchiz anasema kilicho fanya achague tarehe hiyo ni kutokana na kwamba album yake ya kwanza ilidondoka tarehe 11 september mwaka 2001..so alitaka kama kuweka kitu cha kufanana kidogo ...coz atakuwa anatimiza miaka 10 ndani ya Game.lakini pia kama utakuwa na kumbukumbu utajua kuwa ndio siku ya mijengo ya Twin Towers kulipuliwa pande za New york

BIRDMAN APOTEZA KIASI CHA 2 MILLION DOLLARS

Mchzi alikuwa ameweka dau la millioni mbilli kama kamali kwa kujua kuwa timu ya mpiira wa kikapu MIAMI HEATS kutoka miami watashinda finals za NBA lakini haijawezekana..Mshindi wa NBA finals ni DALLAS MAVERICKS kutoka pande za jimbo la DALLAS TEXAS..Dallas wameshinda pointi 105- 95 za Miami HEATS katika mchezo ulio chezwa usiku wa kwamkia leo pande za Marekani... pole sana mzee BIRDMAN..








Saturday, June 11, 2011

JENNIFER HUDSON AKIMBIZWA HOSPITALI

Baada ya kutupia kitu cha performance kwenye show ya Good Morning America.Inasemekana kuwa Mwana dafada huyu alikula msosi tumbo kuanza kumzinguaa .baada ya kuzidiwa Na maumivu ya tumbo ndipo alipo kimbizwa..hospitali moja pande za Newyork City asubuhii ya Ijuuma tarehe 10 juni ili kupata matibabu.kwa maelezo ya daktari alie mtibu na kujaribu kurudisha rudisha hali yake alisema kuwa ilikuwa ni sumu alie kula kwenye msosi...

MWANAE WILL SMITH AITWAE TREY SMITH AMALIZA KITU CHA DIPLOMA

Huyu jama Trey Smith.mwenye umri wa miaka 18 ndio mtoto wa kwanza kati ya watoto wote wa mtu mzima Will Smith...FaMilia nzima kuanzia maza Jada Pinkett-Smith,MA DOGO Jaden na Willow pia walikwepo wakati mchizi anapokea kitu cha Diploma.mara baada ya kumaliza kitu cha High school.. mchizi alikuwa anakamua pande za Oaks Christian high school kule Westlake Village, mjini California.

T.I.P a.k.a CLIFORD HARRIS AWASHUKURU MA FANS WAKE .

Mnyamwezi T.I ametupia kitu cha barua kwa ma fans wake ambao wanamuandikia barua na kuzituma huko gereza la Arkasas alipo fungwa...moja ya vipande toka kwenye hiyo barua kwa maneno yake..T.I anasema hivi..."I’d like to thank you all for the thousands of letters, cards, books, pictures and words of encouragement. I’m truly grateful. I’m sure you already know I’m nearing the end of this chapter of my life, and looking forward to taking all of the things I’ve learned with me while leaving all the rest of the ‘BS’ behind" kwa maneno ya ziada dondoka kwenye tovuti yake T.I kupitia huu mlink..
full letter on his website.

LUPE FIASCO ASEMA HAINA CHA MSAMA WALA NINI KWA RAISI OBAMA

Msani toka pande za 'CHI" TOWN a.k.a "CHICAGO" LUPE FIASCO..asema haina cha kuomba msama kwa raisi wala nini ..kwa mjibu wa LUPE anasema interview ilikuwa na mambo kibao lakini anachoshangazwa nacho ni kwamba ,watu wamesahau kuwa interview ilikuwa ni ya kwake na muziki...ila  kwanini Gumzo lipo kwenye swala la raisi huyo tuu..!!! ..siku kadha hapo nyuma LUPE alihojiwa na kituo cha CBS...na miongoni mwa majibu yake yalisema kuwa . Obama ndio terrorist mkubwa hakuna mwengine..

LIL WAYNE NA BABA YAKE BIRDMAN WASHTAKIWA TENA

Mkali wa young money ..wayne pamoja na dingi yake "Birdman" a.k.a "Baby" wameshtakiwa kwa mara nyingine tena kwa kutolipa watayarishaji wa muziki (producers) wa ngoma za Lil wayne zilizo beng kwa nguvu kwenye album yake ya Carter 3 ,..saivi wamefikia wa nne..producer wa kwanza anaitwa David Kirkwood  ngoma ya "Get money",mwengine ni Jim- josin wa "Lolipop",wa tattu ni Bangladesh wa ngoma kama "Amilli Amilli" na "6foot 7 foot"..na MWISHO KABISA JAMA alie wapelekwa mahakamani anitwa...Deezle Harrison na anadai fine ya kiasi cha dolla za kimarekani millioni 2o kwa kazi alizopiga kwenye ile album ya Carter 3...